Mufindi FM

CARE Tanzania yaadhimisha Siku ya Mtoto wa Kike Mufindi

29 October 2026, 9:09 pm

Diwani wa Viti Maalumu wa Kata ya Mninga, Mh. Asunta Mtende, akizungumza na mwakilishi wa Shirika la CARE Tanzania, Mary Panga, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike.Picha na Kelvin Ayubu.

CARE Tanzania kupitia mradi wa Pesa Yake, Maisha Yake, yaadhimisha Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike Mninga, Mufindi, kwa kutoa elimu kuhusu afya ya uzazi, haki za mtoto wa kike na kupinga ndoa za utotoni.

Na Kelvin Ayubu

Shirika la CARE Tanzania, kupitia mradi wa Pesa Yake, Maisha Yake (Her Money, Her Life), limeadhimisha Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike katika Kijiji cha Mninga, Wilaya ya Mufindi, Mkoani Iringa, kwa kutoa elimu kuhusu afya ya uzazi, ukatili dhidi ya watoto wa kike na namna ya kuzuia mimba za utotoni.

Akizungumza katika maadhimisho hayo, Diwani wa Viti Maalum Kata ya Mninga, Asunta Mtende, amesisitiza umuhimu wa wazazi, walezi, jamii na Serikali kushirikiana katika malezi na ulinzi wa watoto wa kike dhidi ya ukatili na unyanyasaji…

Sauti ya Diwani wa Viti Maalumu wa Kata ya Mninga, Mh. Asunta Mtende.

Kwa upande wake, Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, Hussein Said, na mwakilishi wa CARE Tanzania, Mary Panga, wamewataka wazazi na walezi kuwekeza katika elimu ya watoto wa kike na kuwapatia mwongozo kuhusu afya ya uzazi na kujikinga dhidi ya ukatili.

Sauti ya Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, Hussein Said.

Baadhi ya watoto wa kike na wazazi walioshiriki wamesema elimu waliyoipata imewaongezea uelewa kuhusu haki za watoto wa kike na namna ya kujilinda, huku wakiahidi kuifikisha kwa jamii.

Sauti za baadhi ya watoto wa kike na wazazi walioshiriki katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike

Maadhimisho hayo yaliambatana na maandamano ya wanafunzi katika ofisi za Kata ya Mninga yenye ujumbe, “Tokomeza Ndoa za Utotoni, Wekeza kwa Mtoto wa Kike.” Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike huadhimishwa kila mwaka Oktoba 11 kwa lengo la kuhamasisha haki, usalama na uwezeshaji wa watoto wa kike.