Tarehe kumi Zanzibar kuwa ya kijani
8 August 2024, 4:58 pm
Na Mary Julius
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Zanzibar Abdi Mahmoud Abdi amewataka vijana pamoja na wananchi kuzitumia vizuri barabara na kuzitunza ili ziweze kutumika kwa muda mrefu zaidi.
Amesema hayo Gymkana mara baada ya kupokea matembezi ya baiskeli ya kilomita 25 pamoja na matembezi yaliyoandaliwa na umoja huo ikiwa ni shamrashamra za kuelekea kwenye tamasha la ‘Tunazima taa zote tunawasha za Kijani’ litalalofanyika uwanja wa Amani Mkoa wa Mjini Magharibi. Amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inatumia fedha kujenga barabara zenye kiwango cha kimataifa ili wananchi waondokana na shida ya kukosa huduma muhimu za barabara
Naibu Ametumia nafasi hiyo kuwaasa vijana kuacha kutumia Barabara vibaya hasa wakati wanapoendesha vyombo vya usafiri ili kujikinga na maafa.
Aidha amewaasa vijana kujitokeza kwa wingi katika tamasha la zima zote washa ya kijani ili kumsikiliza makamo mwenyekiti ccm Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mjini kichama TALIB ALI amesema safari hii sio ya tarehe kumi peke yake bali ni muendelezo wa safari ya kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025 octobar.
Aidha amesema leo wamefungua njia zote za mkoa wa mjini kwa ajili ya kupokea wageni wa siku ya tarehe kumi aidha amewata vijana kujipima kwa kujitokeza kwa wingi siku hiyo ya tamasha,
Nae Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Mjini ambaye pia ni Mkuu Wa Mkoa wa Mjini Magharibi Idrisa Kitwana Mustafa amesema wamejipanga kuhakikisha hali ya ulinzi na usalama katika tamasha hilo inakuwepo katika kila maeneo ya mkoa huo.
NAE Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Ali Abdulgulam Hussein amesema vijana ambao wamepewa nafasi ya kuongoza katika serikali ya mapinduzi ya Zanzibar wataendelea kumuunga Mkono Raisi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pamoja na kuunga mkono kampeni ya kuzima zote washa ya kijani.