Zenj FM

Jukwaa la pamoja kurahisisha upatikanaji wa haki

11 November 2024, 5:55 pm

Nae Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Naibu Kamishna wa Polisi Dcp. Zuberi Chembera .

Na Omar Hassan

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais katiba, sheria, Utumishi na Utawala bora anaeshughulikia Katiba na Sheria Mzee Ali Haji amesema uanzishwaji wa jukwaa la pamoja la taasisi za haki jinai itasaidia kutatua changamoto za Taasisi hizo na kuongeza ufanisi katika upatikanaji wa haki za wananchi.

Akizungumza mara baada ya kukutana na Maafisa wa Jeshi la Polisi Kamisheni ya Zanzibar huko Makao Makuu ya Polisi Zanzibar kujadili kuhusu Jukwaa hilo Mzee amesema Ofisi ya Rais katiba, sheria, Utumishi na Utawala bora inaamini kwa kushirikiana kwa Taasisi hizo watamudu kutatua changamoto zinazokwaza utekelezwaji wa sheria.

Sauti ya Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais katiba, sheria, Utumishi na Utawala bora anaeshughulikia Katiba na Sheria Mzee Ali Haji.

Nae Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Naibu Kamishna wa Polisi Dcp. Zuberi Chembera kwa niaba ya Kamishna wa Polisi Zanzibar amesema Jukwaa hilo litalisaidia Jeshi la Polisi kurahisisha utekelezaji wa kusimamia haki.

Sauti ya Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Naibu Kamishna wa Polisi Dcp. Zuberi Chembera