Moto wateketeza hotel Pongwe
8 August 2023, 12:39 pm
Mkuu wa mkoa wa Kusini Unguja amewataka zimamoto kutoa elimu ya kukabiliana na majanga ya moto kwa wananchi.
Na Fatuma
Mkuu wa Mkoa Kusini Unguja Rashid Hadid Rashid ameziagiza mamlaka ya zima moto, shirika la umeme na idara ya maafa kuandaa utaratibu wa kutoa elimu ya mara kwa mara juu ya mbinu za kukabiliana na majanga ya moto kwa wawekezaji wa hoteli za kitalii ili kupunguza adhari zitokanazo na majanga hayo.
Mkuu wa mkoa Hadid ameyasema hayo huko kijiji cha pongwe pwani wilaya ya kati wakati wa ziara ya kuwafariji wamiliki wa hoteli ya Karibu Beach Resort iliyopatwa na janga la kuunguliwa na moto na kusababisha hasara baada ya kuungua moto sehemu za jikoni ,sehemu ya kupokea wageni , paa,na baadhi ya vyumba vya hoteli hiyo.
Amesema hatua hiyo itasaidia kutambua mbinu na hatua zinazofaa kuchukuliwa pale mara majanga yanapotekezea hali iyayopelekea kupunguza hasara kwa kiasi kikubwa kwa wawekezaji zitokanazo na majanga hayo ikiwemo usalama wa wageni na mali zao pamoja na wafanyakazi.
Aidha amemtaka mmiliki wa hoteli hiyo kua na moyo wa subira na serikali iko pamoja na wawekezaji wote na hasa wanaopatwa na majanga kama hayo huku akiwasisitiza kua makini wakati wa kutumia vifaa vinavyotumia nishati ya umeme na gesi ili kujikinga na majanga hayo hasa katika kipindi hicho cha upepo mkali.
Kwa upande wake Kamanda wa polisi mkoa wa kusini unguja Gaudianus .f. Kamugisha amesema jeshi la polisi kwa kushirikiana na wadau mbali mbali wa kukabiliana na maafa watahakikisha wanakaa pamoja kuandaa mikakati madhubuti itakayosaidia kudhbiti majanga hayo ambayo yamekua yakiendelea kuzofisha hali ya ukuaji wa uchumi wa wawekezaji na taifa kwa ujumla.