Uvinza FM

SGR Tabora–kigoma kuchochea maendeleo

26 October 2026, 11:48 am

Picha ya Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa akikagua mradi wa ujenzi wa mradi wawa Reli ya Kisasa (SGR) kipande cha sita kutoka Tabora hadi Kigoma.Picha na mtandao

Treni zitakazotumia reli hiyo zinatarajiwa kusafiri kwa kasi ya kilomita 160 kwa saa, hatua itakayopunguza muda wa safari

Na.Rehema Iddi

Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa, amesema mradi wa Reli ya Kisasa (SGR) kipande cha sita kutoka Tabora hadi Kigoma unatarajiwa kubadilisha maisha ya Watanzania kwa kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii, kurahisisha usafiri wa abiria na usafirishaji wa bidhaa.

Akizungumza Oktoba 25, 2026, wakati akikagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo, Profesa Mbarawa amesema reli hiyo inatarajiwa kukamilika mwaka 2029, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuboresha miundombinu ya usafiri nchini.

Amesema treni zitakazotumia reli hiyo zinatarajiwa kusafiri kwa kasi ya kilomita 160 kwa saa, hatua itakayopunguza muda wa safari, kuongeza ufanisi wa usafirishaji na kufungua fursa zaidi za biashara na uwekezaji katika maeneo yatakayohudumiwa na mradi huo

Sauti ya Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa