Uvinza FM

Udhibiti wa magonjwa ya mlipuko Uvinza wajadiliwa.

22 October 2026, 5:26 pm

Picha ya Katibu Tawala wa Wilaya ya Uvinza, Ndg. James Mkumbo akizungumza na wanakamati. Picha na mwandishi wetu

Tekelezeni majukumu yenu kwa ufanisi, kwakuimarisha ufuatiliaji wa magonjwa ya mlipuko na kutoa elimu sahihi kwa wananchi kuhusu namna ya kujikinga na magonjwa ya mlipuko.

Na. Abdunuru Shafii

Katibu Tawala wa Wilaya ya Uvinza, Ndg. James Mkumbo, akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Uvinza, ameongoza kikao cha Kamati ya Afya ya Msingi ngazi ya Wilaya kilichojadili mikakati ya kudhibiti magonjwa ya mlipuko na kuimarisha ulinzi wa afya ya jamii.

Katika kikao hicho, wataalamu wa afya na wadau wengine wa sekta ya afya wameshauriwa kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi, kuimarisha ufuatiliaji wa magonjwa ya mlipuko na kutoa elimu sahihi kwa wananchi kuhusu namna ya kujikinga na magonjwa hayo.

picha ya washiriki wa kikao hicho. Picha na mwandishi wetu

Aidha, viongozi wa dini wametakiwa kushirikiana na wataalamu wa afya katika kuelimisha na kuikumbusha jamii kuhusu umuhimu wa kuzingatia kanuni za usafi, kutunza afya na kuchukua tahadhari dhidi ya magonjwa ya mlipuko kupitia maeneo yao ya kiutendaji.

Vilevile, ushirikiano kati ya wataalamu wa afya, viongozi wa dini na jamii umeelezwa kuwa muhimu katika kuongeza uelewa wa wananchi, kuzuia kuenea kwa magonjwa ya mlipuko na kuhakikisha jamii inashiriki kikamilifu katika kulinda afya za wananchi wa Wilaya ya Uvinza.