Uvinza FM
Uvinza FM
8 August 2025, 9:23 pm

Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa wilaya ya Uvinza imewataka wananchi kujiepusha na vitendo vya rushwa vinavyorudisha nyuma maendeleo ya taifa hasa kuelekea uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika octoba 2025.
Na Theresia Damasi
Taasisi ya Kuzuia na kupamabana na Rushwa (TAKUKURU) wilaya ya uvinza mkoani Kigoma imewataka wananchi kujiepusha na vitendo vya rushwa vinavyorudisha nyuma maendeleo ya taifa hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika octoba 2025
Akizungumza na Uvinza Redio Afisa TAKUKURU wilaya ya uvinza Bw. Ibrahimu Mtangoo amesema katika kipindi cha uchaguzi kumekuwa na zoezi la rushwa inayotembea kwa wapiga kura ikiwa katika namna tofauti ambazo lengo lake ni wanasiasa kujinufaisha ili kupata uongozi ambapo emeeleza maana ya rushwa na viashiria vyake.
Sauti ya Afisa Ibrahim Mtangoo
Bw.Mtangoo amesema kujihusisha na vitendo vya rushwa kwa kutoa au kupokea rushwa ni kinyume na sheria ya uchaguzi ya mwaka 2024 ambayo imeonyesha makosa na adhabu kwa atakayejishughulisha na vitendo hivyo katika kipindi cha uchaguzi ambapo ameeleza namna ambavyo baadhi ya wananchi kushindwa kutoa taarifa jambo ambalo linarudisha nyuma maendeleo.
Sauti ya Afisa Ibrahim Mtangoo
Ameongeza kwa kusema kwamba mgombea anapaswa kuzingatia kanuni na miiko ya uchaguzi ili kujiepusha na rushwa ambapo wagombea wenyewe hutoa bila kuombwa na zipo zingine ambazo hutolewa kwa sababu wananchi wenyewe huhitaji jambo ambalo ni kinyume na sheria.

Sauti ya Afisa Ibrahim Mtangoo
Aidha Bw. Mtangoo amesema vitendo vya rushwa katika uchaguzi vinamnyima haki mpiga kura ya kumchagua kiongozi anayemhitaji, vinakwamisha maendeleo kwani kiongozi aliyechaguliwa kwa rushwa anaishia kujilimbikizia mali kurejesha fedha na gharama alizotumia, udhalilishaji wa wananchi kwa kulinganishwa thamani zao na pombe vyakula na vitu vidogovidogo wanavyopatiwa na jamii kukosa huduma za msingi na maendeleo.
Sauti ya Afisa Ibrahim Mtangoo
Hata hivyo Bw. Ibrahim Mtangoo amesisitiza kwa kusema kuwa kila mmoja ana jukumu la kuzuia, kukataa rushwa ambaye ni adui wa haki licha yaTAKUKURU wenyewe kuwajibika katika kuzuia na kupambana na rushwa ambapo unaweza kutoa taarifa katika ofisi za TAKUKURU wilaya ya Uvinza kwa kupiga simu kupitia namba 0738150109 na kwa makao makuu unaweza kupiga kupitia namba113kwa atakayebainika na kujihusisha na rushwa.