Uvinza Fm

Ukosefu wa maji wawaliza wananchi

20/05/2021, 7:27 pm

Na,Editha Edward

Wananchi wa kijiji cha Ruchugi wilayani uvinza mkoani kigoma wameiomba serikali iwatengenezee magati ya maji waliyoyaweka ili maji yaweze kutoka na kuondokana  na adha wanayopata  ya kutembea umbali mrefu kufuata maji

Miongoni mwa gati lililotelekezwa

Wakizungumza na redio uvinza fm wananchi  wa kijiji hicho RUKMAN , HILDA ,NA NEEMA wamesema  changamoto ya maji imekuwa ni kero kwani maji wanayanunua kwa dumu moja  shilingi miambili hamsini hadi miatatu

Sauti za wananchi

Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji hicho bw.RAMADHAN KAYUNGIRO amesema jambo hilo wameshaliongea kwenye kikao chao cha ndani hivyo amewaomba wananchi wa kijiji hicho wawe na subira ili maji yaweze kupatikana

Sauti ya Mwenyekiti

Aidha bajeti ya mwaka wa fedha 2020/2021 bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania  lilipitisha bajeti ya maji nchi nzima zaidi ya bilioni miasita.