Uvinza Fm

Kigoma: Serikali kuwachukulia hatua wazazi wasiowapeleka watoto shule

03/07/2023, 12:55 pm

Kutokana na wanafunzi kutojiunga na masomo ya sekondari na wengine kuchelewa kujiunga na masomo, serikali yaahidi kuendelea na zoezi la kuwakamata wazazi wanaokiuka amri hiyo kwa kutumia sheria mbalimbali

Picha ya Afisa Elimu mkoa wa Kigoma Paulina Ndigeza wa katika na baadhi ya viongozi akiongoza kikao cha wazazi katika tathmini ya mahudhurio ya wanafunzi wa shule za sekondari.

Na Glory Kusaga

Changamoto ya baadhi ya wazazi kutokuwa na mwamko wa kuwapeleka watoto wao shule imesababisha baadhi ya wanafunzi mkoani Kigoma kushindwa kuripoti shuleni baada ya kufaulu kwenda elimu ya sekondari

Baadhi ya wazazi wa wanafunzi mkoani Kigoma wakiwa katika kikao kilichoongozwa na Afisa Elimu wa mkoa wa Kigoma

Akibainisha hali hiyo Afisa Elimu mkoani Kigoma Paulina Ndigeza amesema wapo baadhi ya wazazi ambao hawana mwamko wa kuwapeleka watoto shule na kuwapatia haki yao ya kielimu hivyo huwaficha  wanafunzi hao.

Amesema halmashauri ambayo kuna  utoro kwa asilimia kubwa ni halmashauri ya wilaya ya Buhigwe huku akikisitiza kuwa wataendelea na zoezi la kuwakamata kwa kutumia sheria mbalimbali kwa  wazazi wote ambao wanachangia hali hiyo.

Sauti ya Afisa Elimu mkoa Kigoma Paulina Ndigeza

Mpaka kufungwa  kwa dirisha la usajili Machi 31 mwaka huu mkoa wa Kigoma kwa wanafunzi waliofanikiwa kuendelea na shule ya sekondari walioripoti ni 40,738 huku idadi ya waliofaulu ilikuwa ni  44,090.