Uvinza Fm

Serikali yaahidi kuwalinda raia na mali zao

27/05/2021, 5:32 pm

Na,Rosemary Bundala

Serikali imesema inaendelea kuhakikisha usalama wa raia na mali zao unaendelea kuimarika na kuhakikisha kuwa wananchi wanaendelea na shughuli zao za kila siku kwa amani na utulivu

waziri mkuu Kasimu Majaliwa

Hayo yamejiri leo bungeni  jijini Dodoma wakati  waziri mkuu  Kassim Majaliwa alipokuwa akijibu swali la mbunge wa makete mh Festo Richard Sanga lililohoji je ni ipi  kauli  na maelekezo ya serikali dhidi ya vitendo vya uhalifu vinavyoendelea katika taifa letu

Sauti ya Waziri mkuu Kassimu Majaliwa

kwa upande mwingine mh waziri kassim majaliwa amesema anavipongeza vyombo vyote vya dola nchini kwa kuendelea kufanya kazi kwa juhudi katika kuhakiksha usalama wa  wananchi na mali zao unaendelea

Sauti ya Waziri mkuu Kasimu Majaliwa

Katika hatua nyingine waziri mkuu amesema  ni jukumu la kila mtanzania kuhakikisha kuwa anashiriki kikamilifu kwenye ulinzi wa nchi pale anapoona  kuna dalili za upotevu wa amani ni vyema kutoa taarifa kwenye vyombo vya ulinzi

Sauti ya Waziri mkuu kasimu majaliwa

Bunge limeeendelea leo jijini Dodoma ambapo wizara mbalimbali zimekwisha wasilisha bajeti zake .