Uvinza FM

Dc Buhigwe asisitiza ubora na ukamilishaji kwa wakati mto luiche

30 July 2026, 6:28 pm

Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe, Kanali Michael Ngayalina akishiriki katika kubeba mawe kwenye ujenze wa mto luiche. Picha na Afisa habari wa halmashauri

kuongeza juhudi na kuhakikisha ujenzi unakamilika kwa wakati uliopangwa

Na. Abdunuru Shafii

Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe, Kanali Michael Ngayalina, amefanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa daraja linalovuka Mto Luiche, unaotenganisha Kijiji cha Kinazi na Kijiji cha Nyamihanga kilichopo Kata ya Janda. Daraja hilo ni kiungo muhimu kinachounganisha Kata za Kinazi na Munzeze na linatarajiwa kuboresha mawasiliano na usafiri katika eneo hilo.

Akizungumza na mkandarasi anayetekeleza mradi huo, Kanali Ngayalina amemtaka kuongeza juhudi na kuhakikisha ujenzi unakamilika kwa wakati uliopangwa, huku akisisitiza kuzingatia ubora wa kazi ili daraja hilo liweze kutoa huduma ya kudumu kwa wananchi.

Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe, Kanali Michael Ngayalina akikagua ujenzi wa daraja la mto Luiche

Kukamilika, kwa daraja hilo kutarahisisha usafiri na usafirishaji kati ya vijiji vya Nyamihanga, Kirungu, Munzeze na Kishanga kuelekea Wilaya ya Kigoma na Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe, hivyo kuchochea biashara, huduma za kijamii na maendeleo ya wananchi kwa ujumla.