Uvinza FM
Uvinza FM
10 September 2026, 1:00 pm

vijana kuwa mstari wa mbele katika kulinda amani, umoja na mshikamano wa kitaifa
Na. Abdunuru Shafii
Takribani vijana 550 kutoka maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Uvinza wameshiriki Kongamano la Vijana Wilaya ya Uvinza, lililolenga kuwapa nafasi ya kujadili fursa, changamoto na masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo yao.
Katika kongamano hilo, vijana walijadili mada mbalimbali zikiwemo Amani, Umoja na Mshikamano wa Kitaifa; Uzalendo na Uadilifu; Fursa za Kiuchumi; pamoja na Afya na Afya ya Uzazi.\

Akizungumza katika kongamano hilo, Mkuu wa Wilaya ya Uvinza, Mhe. Dinah Mathamani, amewataka vijana kuwa mstari wa mbele katika kulinda amani, umoja na mshikamano wa kitaifa, akisisitiza kuwa ushiriki wao ni muhimu katika kufikia matarajio ya maendeleo ya jamii na taifa.
Kongamano hilo limewakutanisha vijana pamoja na wadau mbalimbali yakiwemo mashirika yasiyo ya kiserikali,Jeshi la polisi na wataalamu wa afya na maendeleo ya jamii kwa ajili ya kubadilishana mawazo, kuhamasishana na kujenga ushirikiano katika kutambua na kutumia fursa zilizopo kwa ajili ya maendeleo ya vijana na Wilaya ya Uvinza kwa ujumla.
