Uvinza FM

Dc amsimamisha kazi mwenyekiti wa mtaa uuzaji eneo la shule

14 April 2026, 2:15 pm

Picha ya eneo la shule lililouzwa na mwenyekiti

polisi mkamateni mwenyekiti huyo na kumfungulia mashtaka ya tuhuma za kuingilia na kuuza eneo la shule

Na Abdunuru Shafii

Mkuu wa wilaya ya Kigoma Dr. Rashid Chuachua amemsimamisha uongozi mwenyekiti wa mtaa wa mgeo kata ya Buhanda Manispaa ya Kigoma Ujiji Azizi Ibrahim huku akitoa maelekezo kwa polisi kumkamata mwenyekiti huyo na kumfungulia mashtaka ya tuhuma za kuingilia na kuuza eneo la shule ya msingi mgeo manispaa ya Kigoma Ujiji mkoani Kigoma.

Dr. Chua Chua alitoa maagizo hayo alipotembelea eneo hilo la shule kufuatia kupata taarifa kutoka kwa vyanzo mbalimbali ya kuwepo kwa tuhuma za kuingiliwa kwa eneo la shule hiyo na kuuzwa kwa mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Atanas Noeli huku maelekezo ya serikali kupitia afisa mtendaji wa kata ya mgeo ya kusimamisha ujenzi huo yakipuuzwa.

sauti ya Mkuu wa wilaya ya Kigoma Dr. Rashid Chuachua

Awali, Afisa Mtendaji wa Kata ya Buhanda, Zeenat Ambikai, alisema eneo hilo liliuzwa mwaka 2021, lakini ujenzi ulianza Januari mwaka huu, licha ya shule hiyo kuanzishwa tangu mwaka 2006.

Pia,  Aliyekuwa Mwenyekiti wa Mtaa wa Mgeo Kata ya Buhanda Azizi Ibrahim amesema eneo hilo lilikuwa chini ya wananchi na limeuzwa likiwa nje ya eneo la shule hiyo ya msingi.

sauti ya Mwenyekiti wa Mtaa wa Mgeo Kata ya Buhanda Azizi Ibrahim