Uvinza FM

wanawake wajawazito watakiwa kuhudhuria klinik kuepuka matatizo ya uzazi

5 May 2025, 11:41 pm

Mkunga(Nesi) wa kituo cha afya uvinza akiwa kwenye seminar ya utoajia elimu juu ya masuala ya uzazi .Picha kutoka maktaba

Madhara mengi yanaweza kujitokeza endapo mama mjamzito atafika kwa kuchelewa hospitalini siku ya kujifungua.

Na Theresia Damasi.

Ikiwa ni siku ya Mkunga Duniani Kituo cha Afya uvinza wilayani uvinza kimewataka akina mama wajawazito kuhudhuria clinik mapema pale tu wanapogundua ni wajawazito ili kuodokana na changamoto za uzazi wakati wakujifungua ikiwemo upungufu wa damu.

Hayo yameelezwa na Nesi (Mkunga )Lille Daniel wakati akizungumza na uvinza fm katika kipindi cha kumekucha ambapo amesema kuna madhara mengi yanaweza kujitokeza endapo mama mjamzito atafika kwa kuchelewa hospitalini siku ya kujifungua ambapo ni hatari kwake na kwa mtoto pia.

Sauti ya Lille Daniel mkunga1

Sambamba na hayo Mkunga huyo amesema changamoto wanazopitia ni pamoja na watoto wanaokuja kujifungua wakiwa chini ya umri wa miaka kumi na nane(18) jambo ambalo ni hatari kwa sababu via vya uzazi bado ni vidogo.

Sauti ya Lille Daniel mkunga 2

Aidha  Mkunga Lille Daniel ametoa ushauri kwa jamii kuzingatia elimu inayotolewa na wahudumu wa afya juu ya masuala ya uzazi  na kuepukana na mimba za utotoni.

Kwa upande wake Sara Daniel ambaye ni mama mjamzito amewashukuru wakunga wote huku akiwaomba waendelee kutoa elimu kwa jamii juu masuala ya uzazi bila kuchoka.

Hata hivyo Maadhimisho ya siku ya mkunga duniani yanafanyika mkoani Shinyanga ambapo yametanguliwa na utoaji wa huduma za afya bila malipo kwenye viwanja vya zimamoto manispaa ya Shinyanga huku Mgeni Rasmi akiwa ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dk.Seif Shekalaghe ambapo kauli mbiu ni ”Mkunga ni Nguzo Muhimu katika kila Janga.”