Utalii waongezeka hifadhi ya Ruaha baada ya kupungua kwa covid 19
09/09/2021, 5:44 pm
Na,Glory Paschal
Imeelezwa kuwa katika Kipindi cha Mlipuko wa Ugonjwa wa Corona awamu ya kwanza na ya pili hali ya watalii kutembelea hifadhi za Taifa Ikiwemo Ruaha ilipungua ikilinganishwa na wakati huu ambapo watalii wameanza kujitokeza kwa wingi kutembelea hifadhi hiyo
Hayo yamebainishwa na Afisa Uhifadhi Kitengo cha Utalii AHMED NASSORO Kutoka Hifadhi ya Taifa ya Ruaha alipotembelewa na waandishi wa habari wanawake kutoka mikoa tofauti hapa Tanzania, ambapo amesema kwasasa watalii wameongezeka kwani wageni 500 hadi elfu 5000 kwa mwezi hutembelea hifadhi hiyo
HALIMA KIWANGO mhifadhi kitendo cha Ekolojia katika Hifadhi ya Taifa Ruaha amesema changamoto kubwa katika hifadhi hiyo imekua ni kukauka kwa maji kwenye mto hasa nyakati za kiangazi hali inayopelekea kupoteza uasilia wa hifadhi hiyo pamoja na wanyama hivyo kuwaomba wananchi waliopo pembezoni kulinda vyanzo vya maji huku hifadhi ikiendelea na juhudi ya kuhakikisha wanaunusuru mto huo
Nae mratibu wa waandishi wahabari wanawake Tanzania bi MARY MWAKIBETE na wadau wengine wa utalii wamesema juhudi za kuhamasisha jamii kutambua umuhimu wa vivutio vya utalii na kuwekeza sehemu mbalimbali itasaidia kuinua uchumi wa nchi kwa ujumla na watu kujitokeza kutalii katika vivutio mbali mbali
Hifadhi ya Taifa ya Ruaha ilianzishwa Mwaka 1910 ikiitwa Saba Game Reserve na baada ya kuboreshwa na kuongezewa maeneo kuwa na uwezo wa kuhifadhi Tambo ilibadilishwa jina mwaka 1964 na kusajiliwa rasmi kuwa hifadhi ya Taifa ya Ruaha ikiwa na ukubwa Kilomita elfu 20,226 na kuifanya hifadhi hiyo kuwa ya pili kwa ukubwa Tanzania.