Uvinza Fm

Serikali yajipanga kujenga mwalo wa kisasa

18/10/2021, 7:24 pm

Na,Glory Paschal

Naibu wa Waziri wa Uvuvi na mifugo ABDALLAH ULEGAamesema Serikali imejipanga kujenga mwalo wa kisasa wa Katonga Manispaa ya Kigoma Ujiji ili wavuvi wapate sehemu Ya kuanika dagaa na kiwanda cha kusindika dagaa.

Mh. ULEGA amesema hayo akiwa Katika ziara ya siku mbili mkoani kigoma na kueleza kuwa serikali inajiandaa kuyainua mazao ya uvuvi na kuwa ya kimkakati

Sauti ya naibu waziri wa uvuvi na Mifugo

Awali akisoma risala mbele ya Naibu waziri,  Mwakilishi wa chama cha wavuvi Kigoma amesema licha ya serikali kuweka mazingira rafiki kwa wavuvi bado wanakabiliwa na changamoto ya kuibiwa vifaa vya uvuvi na ukosefu wa mikopo ya kuendeshea shughuli za uvuvi

Sauti ya msoma risala

Baadhi ya wananchi Mkoani Kigoma wamesema serikali kuanza kujenga mwalo wa dagaa utasaidia kupata sehemu za kuanika dagaa na kuepuka usumbufu wa dagaa kuoza na kukosa thamani ya ushindani kwenye soko la ndani na nje ya nchi.

Sauti za wananchi