Uvinza Fm

Jeshi la polisi latakiwa kufanya kazi zao kwa weledi

24/06/2021, 7:31 pm

Na,Glory Paschal

Watendaji wa Jeshi la polisi pamoja na mahakama Mkoani Kigoma wametakiwa kufanya kazi zao kwa weledi ili kutokomeza mimba za utotoni

Aliyesimama ni Katibu tawala kigoma Rashid Mchatta

Hayo yameelezwa na Katibu Tawala  Mkoani hapa Rashid Kassim Mchatta katika mkutano wa utetezi kuhusu haki za watoto ulioandaliwa na Shirika la We World  kuangazia mimba za utotoni na madhara yake Mkoani hapa

Amesema baadhi ya  wazazi wamekuwa wakitengeneza mianya ya rushwa kwa watuhumiwa na kupelekea kesi nyingi kufutwa

Sauti ya katibu Tawala kigoma

Kwa upande wake Afisa maendeleo Mkoani Kigoma Msafiri Nzunuri amesema endapo jamii itashirikiana vyema tatizo hili la mimba za utotoni litafikia ukomo mkoani hapa

Sauti ya Afisa maendeleo Kigoma

Nae Mchungaji Justin Sologo kutoka Umoja wa Makanisa Mkoani Kigoma amesema mimba pamoja na ndoa za utotoni zitatokomezwa pale tu jamii itakapofuata taratibu zilizowekwa na Serikali kuhusu umri sahihi wa kuolewa na kubeba ujauzito kwa wanawake

Sauti ya mchungaji

Aidha  jamii ikishirikiana kwa pamoja ina uwezo wa kutokomeza mimba za utotoni, na kwa mwaka 2020 Mkoa wa Kigoma ulikuwa na asilimia 20 ya mimba za utotoni na kati ya hizo  wanafunzi 25 wa shule za msingi hawakufanya mtihani wa kuhitimu kutokana na kuwa wajawazito