Uvinza FM

Walimu na wanafunzi wa shule za sekondari wapewa elimu ya kilimo

1 May 2026, 12:36 am

Afisa kilimo bi. Elina akitoa elimu ya kilimo cha bustani kwa walimu na wanafunzi wa shule za sekondari. Picha Na. Halmashauri

Fuateni kanuni bora za kilimo cha bustani ili kuhakikisha uzalishaji endelevu wa mbogamboga pamoja na kuimarisha lishe bora kwa wanafunzi.

Na. Abdunuru Shafii

Afisa Kilimo kutoka Halmashauri ya Mji Kasulu anayeshughulikia mazao ya bustani Bi. Elina Alphonce amefanya ziara katika shule za sekondari Kigoma Grand na Ruhita kwa lengo la kukagua na kutoa elimu kuhusu kilimo cha mbogamboga shuleni.

Katika ziara hiyo, Bi. Elina amewahimiza walimu na wanafunzi kuzingatia kanuni bora za kilimo cha bustani ili kuhakikisha uzalishaji endelevu wa mbogamboga pamoja na kuimarisha lishe bora kwa wanafunzi.

Kwa upande wao, walimu na wanafunzi kutoka shule hizo wameshukuru kwa elimu waliyoipata na kuahidi kuendelea kushirikiana na Halmashauri katika kuboresha na kuendeleza bustani zao kwa kuzingatia ushauri unaotolewa.

Halmashauri ya Mji Kasulu inaendelea kuunga mkono juhudi za Serikali kwa kuhimiza taasisi za elimu kuwekeza katika kilimo cha bustani kama njia ya kujenga uelewa wa lishe bora Shuleni.