Uvinza Fm

KUWASA wakanusha kuwabambikizia bili za maji wateja

12/05/2021, 4:40 pm

Na,Glory Paschal

Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Manispaa ya Kigoma Ujiji, KUWASA wamekanusha taarifa  iliyotolewa na Mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na Maji Ewura kuwa wamekuwa wakiwabambikiza bili za maji wateja

Akizungumza  na Waandishi wa habari Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo Bw. Josephati  Rwegasila amekiri  kuwepo na  baadhi ya watumishi wasiowaaminifu kwa mwaka jana  na tayari wameshawachukulia hatua

Amesema ili kuondoa changamoto hiyo tayari mamlaka imeanza kutumia mfumo mpya ambao umeanza mwaka huu tofauti na mfumo wa awali

Sauti ya kaimu Mkurugenzi Kuwasa

Naye Kaimu Meneja wa biashara wa Mamlaka ya maji Godfrey Robini amesema mfumo huo mpya umekuwa ukimpa taarifa mteja ili aweze kuhakiki taarifa hizo kabla ya kupatiwa bili

Sauti ya Kaimu Meneja wa biashara

Nao baadhi ya wateja wamesema mfumo huo wa kubambikiwa bili kubwa za maji upo jambo ambalo limekuwa likisababisha wananchi kutumia gharama kubwa kulipia bili hizo

Sauti za Wananchi