Uvinza FM
Uvinza FM
14 April 2026, 11:47 pm

Nitaweka mkazo katika kuboresha huduma ya utoaji wa maji safi na salama kwa wananchi wa Kigoma Ujiji
Na. Abdunuru Shafii
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kigoma (KUWASA), Dkt. Christopher Nditi, amefanya kikao na watumishi na kueleza vipaumbele vyake katika kuboresha utendaji wa taasisi hiyo.
Akizungumza katika kikao hicho, Dkt. Nditi amesema atajikita katika kuimarisha hali na maslahi ya watumishi ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku. Amesema watumishi ni nguzo muhimu katika kufanikisha utoaji bora wa huduma ya maji kwa wananchi, hivyo ni lazima kuweka mazingira rafiki ya kazi.
Sambamba na hilo, amebainisha kuwa ataweka mkazo katika kuboresha huduma ya utoaji wa maji safi na salama kwa wananchi wa Kigoma Ujiji, kwa kuhakikisha upatikanaji wake unaimarika na kuwa wa uhakika zaidi.
Aidha, Dkt. Nditi amesisitiza umuhimu wa kukabiliana na changamoto ya upotevu wa maji, akieleza kuwa juhudi za makusudi zitafanyika kutafuta suluhu endelevu. Miongoni mwa mikakati iliyotajwa ni pamoja na ukarabati wa miundombinu chakavu ya Bomba pamoja na kudhibiti na kutokome
