Uvinza FM

Wananchi Kigoma kunufaika na matibabu bingwa na bobezi

20 October 2026, 11:26 am

Picha ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Balozi Simon Nyakoro Sirro.Picha na Mtandao

Wananchi wa Kigoma wamepata fursa muhimu ya kuwaona wataalamu wa afya na kupata matibabu karibu na maeneo yao.

Na Rehema  Iddi

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Balozi Simon Nyakoro Sirro, amezindua rasmi Kambi ya Matibabu ya Madaktari Bingwa na  Bobezi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni, inayolenga kutoa huduma za matibabu kwa wananchi wa Mkoa wa Kigoma na maeneo jirani.

Kambi hiyo imezinduliwa Oktoba 19, 2026, na itaendelea kwa siku tano hadi Oktoba 23, 2026, huku madaktari bingwa kutoka taasisi mbalimbali za afya wakishiriki kutoa huduma kwa wananchi.

 Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Balozi Sirro amesema wananchi wa Kigoma wamepata fursa muhimu ya kuwaona wataalamu wa afya na kupata matibabu karibu na maeneo yao, bila kulazimika kusafiri kwenda mikoa mingine.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Balozi Simon Sirro