Uvinza FM
Uvinza FM
19 October 2026, 11:36 am

kaya hizo kuorodheshwa mara moja ili ziweze kupangiwa makazi mapya katika maeneo yaliyotengwa rasmi nje ya eneo hilo la hifadhi.
Na. Rehema Iddi
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Balozi Simon Sirro, ameiagiza Serikali ya Wilaya ya Kasulu kuondoa kaya zaidi ya 400 zilizovamia na kuanzisha makazi holela ndani ya kitalu cha uwindaji wa kitalii cha Makere Forest Reserve, iliopo katika mpaka wa wilaya za Kasulu na Uvinza.
Akitoa agizo hilo, Balozi Sirro ameelekeza kaya hizo kuorodheshwa mara moja ili ziweze kupangiwa makazi mapya katika maeneo yaliyotengwa rasmi nje ya eneo hilo la hifadhi. Hatua hiyo inalenga kuhakikisha wananchi wanapata makazi salama huku taratibu za kuondoa makazi yasiyoruhusiwa ndani ya eneo la hifadhi zikitekelezwa.
Hatua hiyo pia inalenga kuimarisha ulinzi wa rasilimali za misitu na wanyamapori pamoja na kuhifadhi maeneo yaliyotengwa kwa shughuli za uwindaji wa kitalii. Serikali ya Wilaya ya Kasulu inatarajiwa kutekeleza agizo hilo kwa kuzingatia utaratibu wa kuwapatia wananchi hao maeneo mbadala ya makazi.