Uvinza FM

Elimu ya matumizi ya kilimo bora cha kisasa

13 October 2026, 11:12 am

Bwana shamba wa Seedco Shaini Misani akiwa kwenye kipindi cha kumekucha cha Uvinza Fm
.picha na Fance Alphonce

matumizi ya mbegu bora, kuzingatia muda sahihi wa kupanda, maandalizi ya shamba na kufuata ushauri wa wataalamu

Na. Rehema Iddi

Wananchi wa Wilaya ya Uvinza na Mkoa wa Kigoma kwa ujumla wametakiwa kuzingatia matumizi ya kilimo bora na cha kisasa, pamoja na kufuata kanuni sahihi za kilimo, ili kuongeza tija na uzalishaji wa mazao.

Wito huo umetolewa na Afisa Mauzo wa SeedCo, Mbaya Terito, pamoja na Bwana Shamba wa SeedCo Wilaya ya Kasulu, Shaini Misana, walipokuwa wakizungumza katika kipindi cha Kumekucha kinachorushwa na Uvinza FM. Afisa mauzo mesema matumizi ya mbegu bora, kuzingatia muda sahihi wa kupanda, maandalizi ya shamba na kufuata ushauri wa wataalamu ni miongoni mwa hatua muhimu zinazoweza kumsaidia mkulima kupata mavuno yenye tija na kuongeza kipato

Sauti ya afisa mauzo, Mbaya Terito

Kwa upande wake bwana shamba  Shaini Misani amesema ili kufahamu kama mbegu ni ya Seedco mkulima anapaswa kuhakiki mbegu  pindi anapo kwenda dukani kununua kwa  kwa kuthibitia kwa kuangalia  bacod.

Sauti ya bwana shamba  Shaini Misani