Uvinza FM
Uvinza FM
9 October 2026, 3:07 pm

Na. Rehema Iddi
Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Luteni Kanali Joseph Athanas Murimi ameahidi kuendeleza mazuri yote yaliyofanywa na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo, Kanali Isaac Mwakisu, kuboresha yale yanayohitaji maboresho na kuongeza kasi ya uwajibikaji katika utekelezaji wa majukumu.
Ameyasema hayo wakati wa hafla ya makabidhiano ya Ofisi iliyofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, ambapo amebainisha kuwa kipaumbele chake kitakuwa kulinda amani, usalama na utulivu sambamba na kuhakikisha changamoto za wananchi zinatatuliwa kwa wakati.