Uvinza FM
Uvinza FM
16 November 2026, 11:33 am

Pampu hizo zinalenga kuwawezesha wakulima kufanya shughuli za kilimo kwa uhakika zaidi, hususani katika maeneo ambayo yamekuwa yakikabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa maji.
Na. Rehema Iddi
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Balozi Simon Sirro, amesema Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imegawa pampu 75 za umwagiliaji kwa wakulima waliojiunga katika vikundi 63 mkoa wa kigoma, ikiwa ni hatua ya kuimarisha kilimo cha umwagiliaji na kupunguza utegemezi wa mvua.
Amesema ugawaji wa pampu hizo unalenga kuwawezesha wakulima kufanya shughuli za kilimo kwa uhakika zaidi, hususan katika maeneo ambayo yamekuwa yakikabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa maji kwa ajili ya uzalishaji wa mazao.
Kwa mujibu wa Mkuu huyo wa Mkoa, pampu hizo zinatarajiwa kuongeza eneo la kilimo cha umwagiliaji kwa takribani hekta 1,593 mkoani Kigoma.
Ameeleza kuwa hatua hiyo itawawezesha wakulima kuzalisha mazao katika misimu mbalimbali ya kilimo bila kutegemea mvua pekee, hali inayotarajiwa kuongeza uzalishaji wa mazao.
Aidha, amesema kuongezeka kwa uzalishaji kutachangia kuimarisha kipato cha wakulima pamoja na usalama wa chakula kwa wananchi wa Mkoa wa Kigoma.