Uvinza FM

wahamiaji haramu 34 wakamatwa Uvinza

26 November 2026, 4:15 pm

Picha ya wahamiaji haramu walio kamatwa wilaya ya uvinza.Picha na ofisi ya uhamiaji

Kukamatwa kwa watuhumiwa hao ni sehemu ya jitihada za Ofisi ya Uhamiaji katika kudhibiti uhamiaji haramu, kuhakikisha wageni wanaoingia na kuishi nchini wanafuata sheria na taratibu zilizowekwa, pamoja na kuimarisha usalama wa nchi.

Na.Rehema Iddi

Ofisi ya Uhamiaji Wilaya ya Uvinza, Kanda Maalumu ya Kigoma, imewakamata raia 34 wanaotuhumiwa kuingia na kuishi nchini kinyume na sheria na taratibu za Uhamiaji.

Watuhumiwa hao wamekamatwa Novemba 24, 2026, katika msako iliyofanyika kwenye vizuizi vya Chakulu na Kibaoni vilivyopo Kata ya Uvinza, mkoani Kigoma.