Uvinza FM

Wanahabari redio jamii wakumbushwa maadili ya uandishi

15 October 2026, 7:31 pm

Picha ya Mhariri Mkuu wa jukwaa la habari mtandaoni (radiotadio portal) Hilali Ruhundwa akitoa mafunzo kwa waandishi wa habari wa redio jamii. Picha na Rehema Iddi

Waandishi wa habari wamehimizwa kuzingatia maadili na wajibu wao wa kitaaluma kwa kuandika habari zenye ukweli, usahihi na uwajibikaji.

Na. Rehema Iddi

Waandishi wa habari wamehimizwa kuzingatia maadili na wajibu wao wa kitaaluma kwa kuandika habari zenye ukweli, usahihi na uwajibikaji. Wito huo umetolewa na Mhariri Mkuu wa Jukwaa la Habari Mtandaoni, Hilali Ruhundwa, wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari yaliyofanyika katika ukumbi wa St. Dominic jijini Mwanza.

Sauti ya Hilali Ruhundwa

Katika mafunzo hayo, Ruhundwa amewakumbusha waandishi umuhimu wa kuandika habari zinazohusu watu wenye ulemavu ili kuibua changamoto zao, kutangaza mafanikio yao na kuhamasisha jamii kuheshimu haki na utu wao.

Sauti ya Hilali Ruhundwa

Aidha, waandishi wametakiwa kuepuka lugha za kibaguzi na kuhakikisha watu wenye ulemavu wanapewa nafasi ya kueleza maoni na mahitaji yao. Mafunzo hayo yamelenga kuimarisha weledi wa waandishi katika kuhabarisha jamii kwa kuzingatia ukweli na usawa.