Uvinza FM
Uvinza FM
26 November 2026, 4:59 pm

Mahakama pia imeamuru pikipiki ya mshtakiwa kutaifishwa na kuwa mali ya Serikali pamoja na kulipa fidia ya shilingi 500,000 kwa mhanga.
Na.Rehema Iddi
Mahakama ya Wilaya ya Kasulu imemuhukumu Samwel Maridadi William (19) mkazi wa Mtaa wa Juhudi Kata ya Murusi Wilaya ya Kasulu kifungo cha miaka 20 jela baada ya kupatikana na hatia ya kosa la matumizi mabaya ya kingono (Grave Sexual Abuse) dhidi ya mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka mitano.
Hukumu hiyo imesomwa Novemba 25, 2026 na Hakimu Mkazi Mwandamizi Mheshimiwa Misana M.Majula ambapo Mahakama pia imeamuru pikipiki ya mshtakiwa kutaifishwa na kuwa mali ya Serikali pamoja na kulipa fidia ya shilingi 500,000 kwa mhanga.
Jeshi la Polisi linatoa wito kwa jamii kuwalinda watoto dhidi ya vitendo vya ukatili wa kingono na kutoa taarifa mapema kwa vyombo vya dola ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya wahusika