Uvinza FM
Uvinza FM
28 October 2026, 8:24 pm

Halmashauri itashirikiana na Kamishna Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Kigoma kuboresha huduma za ardhi na kuimarisha ukusanyaji wa mapato.
Na.Rehema Iddi
Kamishna Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Kigoma, Bi. Yuster Z. Byabusha, amewataka wananchi kutumia mfumo wa kielektroniki wa e-Ardhi ili kurahisisha upatikanaji wa hati za ardhi na kuboresha huduma.
Akizungumza wakati wa ziara yake wilayani Kakonko, Bi. Byabusha alisisitiza umuhimu wa kuimarisha utendaji wa maafisa ardhi na kuhakikisha kodi za ardhi zinakusanywa kikamilifu ili kuongeza mapato ya Serikali.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko, Ndaki Stephano Mhuli, amesema Halmashauri itashirikiana na Kamishna Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Kigoma kuboresha huduma za ardhi na kuimarisha ukusanyaji wa mapato.
Katika ziara hiyo, Bi. Byabusha aliambatana na Mpima Ardhi wa Mkoa, Mrisho D. Nineka, pamoja na Afisa Ardhi wa Mkoa, Elias D. Mwazembe. Timu hiyo ilitembelea makao makuu ya Halmashauri na ofisi za ardhi, ambako ilikutana na watumishi kujadili utendaji kazi na utoaji wa huduma za ardhi