Uvinza FM

Waathirika wa mvua Kigoma kupatiwa msaada

2 November 2026, 10:42 am

Picha ya Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Dkt. Rashid Chuachua.Picha na mwamdishi wetu

Serikali imejipanga kuhakikisha wananchi walioathirika wanapata msaada kulingana na mahitaji yao.

Na.Rehema Iddi

Serikali ya Wilaya ya Kigoma imeandaa mpango maalumu wa kuwasaidia wananchi walioathirika na mvua kubwa zilizosababisha madhara katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo, ikiwa ni juhudi za kuwawezesha kukabiliana na athari hizo na kurejea katika hali zao za kawaida.

Akizungumza baada ya kuwatembelea waathirika hao, Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Dkt. Rashid Chuachua, akiwa ameambatana na Kamati ya Usalama ya wilaya, amesema Serikali imejipanga kuhakikisha wananchi walioathirika wanapata msaada kulingana na mahitaji yao.

Amesema Serikali inaendelea kufuatilia hali za waathirika ili kubaini changamoto zinazowakabili na kuweka mikakati ya kuzitatua, akisisitiza kuwa juhudi zinaendelea kuhakikisha wanapata msaada unaostahili.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Kigoma alipotembelea kaya zilizo athiriwa na mvua

Aidha, amewataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya mvua zinazoendelea kunyesha, hususan wanaoishi katika maeneo hatarishi, ili kujikinga na madhara yanayoweza kujitokeza.