Orkonerei FM

Recent posts

22 May 2026, 12:10 pm

Halmashauri ya Arusha yakopesha zaidi ya Tsh mil. 596 bila riba

Na Nyangusi Olesang’ida Halmashauri ya Wilaya ya Arusha imetoa jumla ya Shilingi milioni 596,000,000 kama mikopo isiyo na riba kwa robo ya nne ya mwaka wa fedha 2025/2026, inayolenga kuyawezesha makundi maalum kiuchumi ikihusisha vikundi 18 vya wanawake, vikundi 26…

22 May 2026, 5:32 am

Kunywa damu mbichi hatari kwa afya-Utafiti

Na Dorcas Charles Wafugaji katika Wilaya ya Simanjiro na maeneo mengine nchini wametakiwa kuzingatia usalama wa maziwa na kuacha kabisa utamaduni wa kutumia damu mbichi. Wito huo unafuatia matokeo ya uchunguzi wa sampuli za maziwa uliobaini uwepo wa viashiria vya…

21 May 2026, 1:31 pm

Jamii za kifugaji zatakiwa kutoa kipaumbele katika elimu

Wazazi na walezi, hasa kutoka katika jamii za kifugaji Wilayani Simanjiro, wameshauriwa kubadili fikra na kuwapa watoto wao kipaumbele cha elimu badala ya kuwatanguliza katika shughuli za uchungaji wa mifugo wakati wa masomo. Na Baraka Olemaika Ushauri huo umetolewa kufuatia…

20 May 2026, 1:46 pm

Daktari atuhumiwa kumbaka binti yake wa darasa la saba

Daktari mmoja wa kituo cha afya jijini Arusha anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kumbaka mtoto wake wa kumzaa anayesoma darasa la saba, huku kukiwa na malalamiko kutoka kwa mama mzazi kuwa mtuhumiwa ameachiwa kwa dhamana na upelelezi…

7 May 2026, 11:55 am

Wanahabari watakiwa kuwa vinara wa mapambano dhidi ya katili

Waandishi wa habari na watangazaji wa vipindi vya watoto, malezi, matunzo ya mtoto na familia nchini, wametakiwa kuwa vinara wa kuibua na kufuatilia habari zinazohusu vitendo vya kikatili vinavyofanywa katika jamii. Na Joyce Elius Wito huo umetolewa na wawezeshaji Victor…

24 April 2026, 1:14 pm

Upatikanaji wa maji unavyobadili maisha ya wanawake Simanjiro

Na Isack Dickson Katika Wilaya ya Simanjiro, Mkoa wa Manyara, upatikanaji wa maji safi na salama unaendelea kufungua fursa mpya za maendeleo kwa wanawake. Kupitia kilimo cha umwagiliaji, wanawake wengi sasa wanalima mbogamboga, kuongeza kipato cha familia, kuboresha lishe za…

17 March 2026, 10:01 am

Wananchi terrat waelezwa faida za Mama kujifungulia hospitalini

“Ushauri wangu ni kwamba mama anapoanza kuhisi dalili za uchungu, asisubiri mpaka dakika ya mwisho. Ni vyema awahi hospitalini mapema ili kupata huduma stahiki na kuepuka vifo vya mama na mtoto” Na Baraka Olemaika Akina mama wajawazito nchini wameshauriwa kuhakikisha…

17 March 2026, 9:51 am

Walazimika Kubebwa Mikononi Kuvushwa Korongoni

Walilazimika kubeba mgonjwa kwa shida ili kuvuka korongo hilo baada ya kushindwa kupata usafiri. Na Evanda Barnaba Wananchi wa Kijiji cha Oldonyo, Kata ya Lemooti wilayani Monduli wamelalamikia hali mbaya ya korongo linalowaunganisha na Kijiji cha Lolkisale wakisema limekuwa hatari…

Dira na Dhamira

DIRA:

Kuwa na jamii ya kifugaji yenye uelewa na ufahamu mpana katika maendeleo kupitia upashanaji wa habari

DHAMIRA:

Kuandaa na kurusha vipindi vya kuboresha maisha ya jamii katika elimu, afya, usawa, uongozi na utawala Bora.

Orkonerei FM Redio ni Redio ya jamii iliyopo katika kijiji cha Terrat wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara iliyoanzishwa mwaka 2002 kwa lengo la kuelimisha, Kuhabarisha na kuburudisha jamii za wafugaji na jamii zingine zilizopo katika mkoa wa Manyara,Arusha,Kilimanjaro na mkoa wa Tanga.

Orkonerei FM Redio inapatikana kwa masafa ya 94.3 MHz na kauli mbiu yetu ni “Sauti yako,Sauti ya jamii”