Kauli ya mkuu wa mkoa wa Arusha kuhusu watoto kurejea shuleni
11 January 2024, 1:15 pm
Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania imeendelea kuweka swala la elimu kuwa kipaumbele na kuhakikisha wanafunzi wanasoma katika mazingira mazuri na kuhakikisha wazazi wanawapeleka watoto shule.
Na Nyangusi Olesang’ida
Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongella amewataka wazazi na walezi wa mkoa huo kuhakikisha wanafunzi wote wanaandikishwa shule na kuwataka wazazi kuwajibika kwa nafasi yao kwani tayari serikali imewajibika kwa nafasi yake
Mongella ameyasema hayo wakati akiwa katika ziara yake yakutembelea na kukagua maendeleo ya shule katika mkoa huo
kwa upande wa diwani wa kata ya Olmotonyi halmashauri ya Arusha (Arusha dc) Devid Kinisi amewasihi wazazi na walezi kuwa na ushirikiano mzuri na walimu ili kusaidia maelewano katika ulipaji wa chakula shuleni na kuwataka wanafunzi kuwasili shule walizopangiwa hata na sare za shule zile za msingi.
Baadhi ya wazazi wa mkoa huo wamewashauri wazazi na walezi kuwapeleka watoto shule na kuwaomba walimu kufanya mawasiliano na wazazi kabla ya kuwarudisha wanafunzi kwasababu ya michango.
Naye mwalimu Elifasi Laizer anasema ili kuhakikisha watoto wanapata elimu bora anawasihi walimu na wazazi kuwa na ushirikiano