Radio Fadhila

Siku 16 za Kupinga Ukatili: Jamii Yatakiwa Kutovumilia Vitendo vya Ukatili

26 November 2026, 12:25 pm

Jamii Masasi yatakiwa kutoshiriki kimya pale inaposhuhudia vitendo vya ukatili wa kijinsia, bali kutoa taarifa kwa mamlaka husika ili kukomesha vitendo hivyo.

Na Godbless Lucius

Jamii wilayani Masasi, mkoani Mtwara, imetakiwa kutoa taarifa katika mamlaka husika pale inapobaini matukio ya ukatili wa kijinsia yanayotokea katika maeneo yao ili kusaidia kukomesha vitendo hivyo. Wito huo umetolewa na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mwanzo Lisekese, Zainabu Mtoro, katika mahojiano maalumu yaliyofanyika kupitia kipindi cha Morning Booster kinachorushwa na Redio Fadhila.

Akizungumza katika mahojiano hayo yaliyolenga kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia, Zainabu amesema ukatili wa kijinsia si jukumu la serikali pekee, bali ni wajibu wa kila mwananchi kushiriki katika mapambano hayo kwa kuchukua hatua pale anaposhuhudia vitendo vya ukatili.

Aidha, amesisitiza kuwa jamii haipaswi kukaa kimya mtu anapofanyiwa ukatili, awe mtoto au mtu mzima, bali inapaswa kutoa taarifa kwa vyombo na mamlaka husika ili hatua stahiki zichukuliwe na vitendo hivyo viweze kukomeshwa. nipe caption fupi kupitia hii

Sauti ya