Radio Fadhila

Mshona viatu miaka 30 jela

1 May 2024, 11:50 AM

Na Lilian Martin,

Masasi

Mkazi wa mtaa wa Dodoma Wilayani Masasi Saidi Bakari mwenye umri wa miaka 42 anaye jishughulisha na ushonaji wa viatu ahukumiwa kifungo Cha miaka 30 jela Kwa kosa la Kumbaka Bi Eva chande mkazi wa mtaa huo.

Mtuhumiwa alitekeleza tukio hilo katika maeneo ya nyumbani kwake ambapo alimvutia ndani kwake Bi Eva wakati alielekea bombani kuchota Maji.

Na Kwa upande wa hakimu mkazi Reheme Yunus Iddy na wakili wa serikali mwandamizi Wilayani Masasi aliridhishwa na maelezo ya watoa ushahidi na kumtia hatiani said Bakari na kumuhukumu kifungo hicho.