Radio Fadhila

CCM Mtwara yakagua miradi ya maendeleo Masasi

17 November 2023, 10:02 AM

Masasi

Kamati ya Chama Cha Mapinduzi {CCM} mkoa wa Mtwara, imefanya ziara ya kikazi wilayani Masasi kwa lengo la kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani humo.

Ziara hiyo imeongozwa na katibu wa chama ngazi ya mkoa David Molle, ambapo  walitembelea shule ya msingi Mkuti B na kukagua vyumba vitatu vya madarasa pamoja na matundu ya vyoo wakiwa wilayani humo.

Baada ya ukaguzi wa mradi huo David Molle ametumia nafasi hiyo kuwataka viongozi wa halmashauri kutafuta namna bora ya kujenga uzio katika shule kwa lengo la kuwalinda wanafunzi hao huku wakitakiwa  kutoa nafasi kwa kuwashirikisha wanachi katika miradi mbalimbali.

Pia katika ziara hiyo walitembelea mradi wa shule ya  sekondari kata ya Jida ambao  unatarajia kukamilika hivi karibuni na Januari wanafunzi  wataanza kusoma hapo.