Radio Fadhila
Radio Fadhila
15 April 2026, 12:38

Katika kukuza sekta ya elimu nchini waziri wa ardhi na maendeleo ya makazi Dk Leonard Akwilapo amezidi kugusa baadhi ya shule na kuwapatia vifaa.
Na lilian Martin
Mbunge wa Jimbo la Masasi Mji,Waziri wa Ardhi nyumba na maendeleo ya Makazi, Dk. Leonard Akwilapo, ametoa vitabu 604 vya masomo ya Bookkeeping na Commerce kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mtapika na Shule ya Sekondari Masasi Day, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha elimu na kuongeza ufaulu kwa wanafunzi wa jimbo hilo.

Akigawa vitabu hivyo, Katibu wa Mbunge, Ndugu Shiraji Zaburi, amesema msaada huo ni sehemu ya kuendeleza juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kuboresha sekta ya elimu na kuhakikisha upatikanaji wa elimu bora katika shule za Tanzania.
Aidha, amebainisha kuwa hii si mara ya kwanza Mbunge kusaidia sekta ya elimu, kwani awali aligawa vitabu 3,677 vya masomo mbalimbali katika shule za jimbo la Masasi. Hata hivyo, baada ya kubaini kuwa Shule za Sekondari Mtapika na Masasi Day zinafundisha masomo ya Bookkeeping na Commerce, Mbunge aliona umuhimu wa kuongeza vitabu maalum kwa masomo hayo ili kuhakikisha wanafunzi wanapata rasilimali stahiki za kujifunzia
lakini pia walimu walipata wasaa wakuzungumza na kutoa shukurani zao kwa zawadi ya Vitabu ambavyo wameahidi kuvitumia vizuri
hata hivyo wawakilishi wengine walishukuru juhudi za Waziri wa Aridhi katika kukuza sekta ya elimu