Radio Fadhila

Mnzava aridhishwa utekelezaji wa miradi Masasi na kuizindua

6 June 2024, 19:49

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Ndg. Godfrey Eliakimu Mnzava amezindua miradi mitatu (3) na kuweka mawe ya msingi katika miradi miwili (2), kukagua na kuona miradi miwili (2) Halmashauri ya Mji Masasi mkoani Mtwara.

Mbio za Mwenge wa Uhuru zimepokelewa leo Juni 6, 2024 katika eneo la viwanja vya kijiji cha Mlundelunde kata ya Mumbaka kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Masasi.

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru amezindua mradi wa maji Namatunu, karakana ya utengenezaji wa magari, ujenzi wa jengo la upasuaji Hospitali ya Mkomaindo, ameweka jiwe la msingi katika ujenzi wa vyumba tisa vya madarasa shule kongwe ya msingi Mkomaindo na ujenzi wa barabara ya Top Queen Nyasa Magengeni kiwango cha lami yenye urefu wa Km 0.7 sambamba na kukagua na kuona shughuli za ujasiriamali za vijana wanaotengeneza vifaa vya aluminium na kukagua shamba la miti TFS lenye ukubwa wa ekari 94.57

Mwenge wa uhuru ukiwa Halmashauri ya Mji Masasi umekimbizwa umbali wa km 66.3, na kupita katika tarafa moja, kata kumi, vijiji tisa na mitaa kumi na sita.

Mwenge wa Uhuru umepitia, kukagua, kuzindua na kuweka mawe ya msingi kwenye miradi yote saba ya Halmashauri ya Mji Masasi.