Radio Fadhila

Wazazi washauriwa kunyonyesha mtoto kwa wakati

8 August 2023, 10:45 AM

Mratibu wa lishe Halmashauri ya Mji Masasi Happiness Mlamka ametoa rai kwa jamii ya Halmashauri ya Mji wa Masasi wakiwemo waajiri na kinababa Mkoani Mtwara  kutoa ushirikiano wa kutosha kwa kinamama wanaonyonyesha watoto ili waweze kuwanyonyesha watoto wao katika hali ya utulivu ikiwemo  kuweka mazingira wezeshi ili unyonyeshaji huo ufanyike kwa  tija kwa watoto.

Timu ya lishe kutoka Halmashauri, ya Mji wa Masasi wakiwa katika studio za radio fadhila

Mlamka ametoa rai hiyo wakati akiwasilisha mada ya unyonyeshaji  katika studio za Radio fadhila mapema wiki hii, kama sehemu ya kuadhimisha wiki ya unyonyeshaji ya maziwa ya mama pekee, ambapo kauli mbiu kwa mwaka huu inasema saidia unyonyeshaji wezesha wazazi kulea watoto na kufanya kazi zao za kila siku.

Mlamka akizungumza katika sehemu ya wasilisho lake amesema Baba anapaswa kuwajibika kwa kuweka mazingira wezeshi ili kumfanya Mama aweze kunyonyesha Mtoto wake kwa utulivu bila ya kuathiri hali hiyo ya unyonyeshaji kwa kusema.

Sauti ya Happiness Mlamka – Mratibu wa lishe Halmashauri ya Mji Masasi

Ikumbukwe wiki hii ya unyonyeshaji ya Mama uadhimishwa kila mwaka ifikapo  tarehe 1 mwezi wa nane ya kila mwaka na kilele chake huhitimishwa tarehe 7 ya mwezi huu. Aidha naye kwa upande wake Jesse mhina amesema kina mama wanapaswa kutumia wiki hii vizuri kutokana na umuhimu wa watoto kunyonya maziwa ya Mama pamoja na kujenga uhusiano mzuri kati ya Mtoto na Mama