Radio Fadhila

WAKIHABIMA waitaka jamii kuibua taarifa za vitendo vya kikatili

8 August 2023, 10:59 AM

Afisa vijana kutoka idara ya maendeleo ya jamii  halmashauri ya mji wa Masasi mkoani Mtwara Ebeneza Wisso, ametoa rai kwa wasaidizi wa kisheria kutoka shirika lisilo la kiserikali linalojihusisha na usaidizi wa kisheria katika halmashauri hiyo   WAKIHABIMA, kujikita katika jamii kwa kutoa elimu tambuzi ili jamii ipate uelewa wa kutosha na  kuibua vitendo vya kikatili na kisha kupatiwa usaidizi wa kisheria.

Picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo. Picha na mwandishi wetu

Ebeneza ametoa rai hiyo alipoalikwa na taasisi hiyo kama sehemu ya mgeni rasmi katika mafunzo ya kujengewa uwezo kwa wasaidizi hao wa kisheria  kutoka maeneo mbalimbali ya wilaya ya Masasi yaliyowezeshwa na shirika la International Rescue Committe IRC .

Katika uzinduzi wa mradi wa Kijana Kwanza, ukihusisha vijana kutoka mkoa wa Mtwara ikiwemo wilaya ya Masasi katika kata za Migongo, Jida na Mkuti.

Sauti ya Ebeneza Wisso

Kwa upande wake Saraha Mwaisaka kutoka Idara ya   Maendeleo ya Jamii ambaye pia mratibu wa ofisi ya mashirika yasiyo ya kiserikali NGOS katika halamshauri ya mji wa Masasi akizungumza katika sehemu ya mazungumza yake akaelezea kwanini wasaidizi wa kisheria wamekutana hapo.

Sauti ya Saraha Mwaisaka kutoka Idara ya   Maendeleo ya Jamii

Katika mafunzo hayo ya siku moja wajumbe walishirikishana mada mbalimbali za  masuala ya ukatili na kuzielezea kwa lengo la kupata uelewa wa pamoja akiwemo mratibu wa shirika hilo.