Radio Fadhila

Siku 16 kupinga ukatili Mtwara

11 December 2023, 7:35 PM

Kilele cha maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia mkoa wa Mtwara yamefanyika wilayani Masasi katika uwanja wa Boma na kuongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Mhe. Dkt. Stephen Isaac Mwakajumilo akimwakilisha mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanal Ahmed Abas.

Akiwahutubia wakazi wa Masasi amesema kwa mujibu wa taarifa dawati la ustawi wa jamii mkoa wa Mtwara kwa kipindi cha Januari hadi Septemba 202, jumla ya matukio 1120 yaliripotiwa ikiwemo ya watu wazima 436, wanawake 336 na wanaume 100 na watoto 684.

Maadhimisho siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia

Aidha amesema, “Ndugu zangu jambo lingine ni ma Mwenye na ma Apiamwene wajibu wao wameutelekeza mtoto anapelekwa Jandoni au Unyago akiwa na umri wa miaka mitano anajifunza nini na atarudi na nini. Matokeo yake huko mnamfundisha vitu vikubwa namna ya kulea ndoa kwa maana nyingine tunawahamasisha watoto wadogo waendelea kufanya vitendo ambavyo ni kinyume, Niwasihi mamwenye na wadau wengine popote walipo wanaopambana na hili janga la ukatili wa kijinsia walinde imani zao walinde maadili yao kuhakikisha taifa letu linalejea katika misingi iliyo bora.