Radio Fadhila

Meneja Crdb Masasi akanusha uvumi mkopo wa Mama Samia

8 April 2024, 12:26 PM

mikopo

Meneja wa Crdb Masasi Heriethi Rechengura akanusha upotoshwaji wa taarifa za mikopo inayo tolewa na Crdb Kwa akili ya kuwainua wanawake na kuitwa mikopo hiyo niya Mama Samia.

Bi Herieth amekanusha uvumi huo Kwa kutoa ufafanuzi kuwa mikopo iliyopo Crdb ni mikopo ya wanawake wafanyabiashara Kwa Lengo wa kuwainua na inataratibu zake

amesema amepokea taarifa ya kuwa Kuna watu wanao washawishi wakina mama kujaza fome za kuchukua mikopo ya Mama Samia na wanapofika Benk hapo na kupata taarifa sahihi upelekea hali kuona wametapeliwa kutokana na taarifa walizopata

Nakwa upande wao Moja ya kikundi kilicho hamasika kuchukua mkopo huo kimetoa malalamiko ya kupotezewa muda wao Kwa kufuatilia mkopo ambao mwisho wake umekuwa na majuto kwao

(Laiti ningejua kuwa sio mkopo wa Mama Samia tangu mwanzo nisinge poteza muda wangu maana naona kama nimatapeli tu maana wasingetumia jina la Rais kutushawishi) .alisema mmoja wa kikundi hicho

hataivyo wakina mama hao waliendelea kusisitiza kuwa serikali iingilie kati Kuwatia nguvuni watu hao wanaotumia jina la Mama Samia kushawishi wakina mama kuchukua mikopo ambayo sio ya Mama Samia