Radio Fadhila

Ahaidi kuandika historia nyingine licha ya kuwa historia ndefu

22 April 2024, 5:39 PM

Na Lilian Martin

Ni mwenyekiti wa CCM wilaya Masasi

mwenyekiti wa CCM wilaya ya Masasi Bi Mariam Kasembe ameahidi kuandika historia mpya licha ya kuwa na historia ndefu nyuma uongozi, maumivu na kukatishwa tamaa

amesemakuwa safari yake ya kuongozi ilianza katika ngazi ya mwenyekiti wa Kijiji, udiwani,ubunge hadi kufikia halipo

safari haikuwa rahisi Kuna milima mabonde, na kukwepa mishale mingi wakati mwingine nilipitia haya kutokana na jinsia yangu maana nafasi zingne niligombea na wanaume hivyo ndani yake kulikuwa na maneno ya kashfa matusi na dharau ila nilisimama imara bila kujali.

aliongeza Kwa kusema kuwa jitihada zake na kupenda anachokifanya ndio siri ya mafanikio yake katika uongozi anajivunia nafasi alizowahi kuzitumikia Kwa kuwa ameacha ala zinazompa furaha hata Sasa kama kituo Cha police Lukuledi na vitu vingine

(katika vitu vilivyo umiza moyo Hadi familia yangu na kinishauri niachane na uongozi ni tukio la kuchumewa nyumba moto na kuteketea Kwa Kila kitu kilichokuwepo ndani kama Gar, Trecta na vitu vingine hii ilifanya Hadi familia wakanishauri niachane na siasa japo bado sikuishia hapo,) alisema Kasembe

aliendea kusema kuwa licha ya yote yaliyotolea katika uongozi wake aliona sio mwisho wa safari yake bali ndani yake anatamani kulipia fadhila Kwa chama Cha mapinduzi ndipo alipochukua tena fomu ya kugombea uenyekiti wa chama ambapo pia kulikuwa na mchuano na wanaume waliotaka nafasi hiyo hatimae kuibuka mshindi na kuahidi kuandika historia nyingine kwakuwa bado nguvu anayo.