Radio Fadhila

Madhara yatokanayo na mimba za utotoni-Radio Fadhila

20 March 2021, 6:23 AM

Tatizo la mimba za utotoni limekuwa kubwa duniani na linaongezeka siku hadi siku hasa katika jamii ya uchumi wa chini. Sababu zinazopelekea jamii ya uchumi wa chini kukumbwa sana na tatizo hilo ni ukosefu wa taarifa za afya ya uzazi na umasikini.

Kipindi kilichopita tuliangazia sana chanzo cha mimba za utotoni na sauti za watu mbalimbali zilisikika wakiliongelea tatizo hilo kwa mapana zaidi. Kuna madhara makubwa sana yatakanayo na mimba za utotoni zikiwemo za kiuchumi,kisaikolojia,kiakili na kiafya.

Wataalamu wa afya  ya uzazi wanashauri ili kuepukana na matatizo ya kiafya ni vyema  kupata mimba baada ya kufikisha umri wa miaka 18. Chini ya miaka 18 msichana bdo hajakomaa kiakili na kimwili kuweza kubeba majukumu ya malezi,pia nyonga huwa changa na nyembamba hivyo kutoweza kubeba kiumbe na kusababisha madhara makubwa wakati wa kujifungua.Madhara mengine ya kiafya yatokanayo na mimba za utotoni ni kutokwa na damu nyingi wakati wa kujifungua,Fistula(kutokwa na haja ndogo),kifafa cha mimba na vifo vya mama na mtoto.Mtalamu wa afya anatueleza kwa kina nn madhara ya mimba za utotoni

Kama tulivyosikia mtaalamu wa afya akitueleza madhara yatokanayo na mimba za utotoni.Safari ya Jamii yetu haikuhishia hapo tulifanikiwa kuongea na mhanga ambaye ni binti aliyepata madhara ya kiafya wakati wa kujifungua yeye alipata mimba na umri mdogo hivyo atatueleza madhara gn aliyoyapata

Binti huyo na wengine wengi wanaopitia changamoto kama hzo,Jamii,Taasisi zisizo za kiserikali na wadau kwa ujumla watupasa kushirikiana na Serikali kwa pamoja kupambana na mimba za utotoni ili tufanikishe kupunguza au kutokomeza kabisa. Pia tumeweza kuongea na Mwelimishaji rika Bi Salome Jerome yeye amefana juhudi za kuwaelimisha watoto waliopata mimba mapema na kuwapa elimu ya utambuzi ili waweze kujitambua na kuzuia kutopata mimba ya pili wangali bado wadogo

Na njia kubwa ya kumwepusha mtoto wa kike na mimba za utotoni ni kumsomesha,hvyo jamii hiakikishe mtoto wa kike anabaki shule.Tunaamini kwamba ukimsomesha mtoto wa kike umeikomboa jamii yote.Serikali imefanya juhudi ya kutoa Elimu bure hvyo ni jukumu letu kama jamii kuwapeleka watoto shuleni na kuwahimiza kusoma kwa bidii.

Tunae Mratibu wa Miradi Bw TORAI KIBITI kutoka KIMAS wao wanajishughulisha na masuala mbalimbali ya kijinsia,         hivyo ataweza kutuelezea nini kifanyike ili kumwepusha mtoto na mimba za mapema

Mijadala mingi imepita juu ya mkanganyiko wa umri wa mtoto,Sheria ya mtoto sura ya 21 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2019 mtoto ni yule aliye chini ya miaka 18,na anaruhusiwa kuolewa chini ya umri huo kwa idhini ya wazazi au mahakama.Lakini kesi ya kikatiba ya REBECA GYUMI ya mwaka 2016 kupinga baadhi ya vifungu vya 13 na 17 vya sheria ya ndoa,Mahakama ilitoa hukumu ya bado ijulikane mtoto ni chini ya miaka 18.

Hvyo mpaka sasa Bunge kama mhimili mkuu wa kutunga na kurekebisha sheria haijakaa kurekebisha sheria ya mtoto hivyo kuna changamoto kubwa ya kupambana na ndoa za utotoni ambazo ni chanzo cha mimba za utotoni.Nini maoni ya wadau wa sheria juu ya mkanganyiko huo,Tunae wakili wa kujitegemea ndg FRORENCE MWANAWIMA kutoka NIASSA&CO ADVOCATES iliyopo Masasi Mtwara yeye atatueleza nini mtazamo wa kisheria

Mkanganyiko huo unasababisha wadau wa  kupambana na kutokomeza mimba za utotoni kushindwa kufanya kazi zao kikamilifu kutokana na sheria kutokuwa rafiki.Hivyo kuwa na wimbi kubwa la ndoa za utotoni zinazopelekea mimba za mapema.

Hivyo basi Jamii inatakiwa kutoa Elimu ya Afya ya uzazi hasa pindi anapovunja ungo/balehe.Wazazi/walezi watoe elimu juu ya changamoto atakazokumbana nazo mtoto pindi anapokua balehe na jinsi gani ya kuziepuka.

Pia wazazi/walezi wawalee vema kimadili na kuishi na hofu ya Mungu pia waweze kukaa na watoto wao na kubadilishana mawazo juu ya kukua kwa technologia.Tuache kulaumu mmomonyoko wa maadili ni vyema tukatafuta namna ya kuongea na vijana wetu.