Radio Fadhila

Masasi waonywa kutotumia walemavu kujiingizia kipato

17 November 2023, 10:08 AM

MASASI.

Jamii wilayani Masasi imetakiwa kutowatumia watu wenye changamoto ya ulemavu kama sehemu ya kujiingizia kipato kwani kufanya hivyo ni kosa kisheria.

Wito huo umetolewa na wakili wa kujitegemea wilayani humo Kida Mwangesi, katika studio za Radio Fadhila wakati akiwasilisha mada ya watu wanaoishi na ulemavu katika kipindi cha Ijue Sheria kipindi kinachoruka kila Jumatano ndani ya kipindi cha Amkana Radio Fadhila majira ya saa mbili na nusu asubuhi mpaka saa tatu kamili asubuhi.

KIDA akizungumza katika sehemu ya wasilisho lake amesema,Binadamu wote katika jamii tunawajibu wakuwasaidia Watu wenye ulemavu lakini sivizuri kuwatumia Watu wenye ulemavu kamachombo cha kuingizia mapato kwani kufanya hivyo ni kosa kisheria  kwakusema

Naye kwa upande wake Lightness Masimba ambaye ni hakimu mkazi mfawidhi mahakama ya mwanzo Lisekese wilayani humo amesema sheria hipo na Serikali inatambua hivyo kuimiza jamii yenye ulemavu endapo watafanyiwa vitendo ambavyo vipo kinyume na sheria katika jamii ni budi waviripoti ili vishughulikiwe kwa mujibu washeria.

Kipindi cha Ijue Sheria ufanyika kila Jumatano asubuhi katika Studio zetu ili kuisaidia jamii kuwa nauelewa mpana kuhusu masuala mbalimbali ya kisheria.