Radio Fadhila

Waomba kujitoa katika chama Cha msingi walichopo na kupata chama kipya

22 April 2024, 4:16 PM

Wakulima wakiwa katika kikao

Na Lilian Martin

Masasi

wakulima kutoka vijiji vya Chilimba Lisanje na Misechela vilivyopo Wilayani Masasi wamefanya kikao kilicho hudhuriwa na diwani wa kata hiyo mh.Juma Satma kilicho lenga adhima ya kupata chama Cha msingi kipya na kujiondoa kwenye chama Cha Chiungutwa Amcos ambacho nichama walichopo

wakulima hao ambao pia ni wanachama wa Chiungutwa Amcos ameomba kupata chapata chama kingine katika vijiji hivyo kutokana na changamoto wanazozipata wakati wa ukusanyaji wa mazao galani hadi kufikia malipo

Ikifika kipindi Cha msimu tunakusanya mazao lakini katika ulipaji tunapata changamoto ya kuchelewa kulipwa sisi watu wa vijiji hivi kutokana na ukusanyaji kuwa mkubwa na kushindwa kupata nafasi za mwanzo kuuza mazao yetu. Walisema wakulima hao

pamoja na hayo wachangiaji waliahidi kushirikiana vema na chama watakacho jitoa Kwa kuwa ni swala la maendeleo Kwa chama kazaa chama kingine.