Radio Fadhila

Mkuu wa Wilaya ya Masasi mpya Asisitiza Wananchi kumuunga mkono katika ELIMU na KILIMO.

17 February 2023, 10:42 AM

Mkuu wa Wilaya ya masasi LAUTERI KANONI ameiyomba  jamii ya Masasi imuunge mkona katika mikakati yake ya kuboresha elimu Wilayani humo kwani amekuja na mpango wa kuakikisha kila Shule ya Sekondari ya Kata inajengwa Hosteli ili kuwafanya Wanafunzi waweze kusoma kwa bidii na waweze kufaulu katika Mitihani yao ya mwisho yakuhitimu kidato cha nne.

Mbali nahilo pia Kanoni ameiyasa jamii ya Masasi kubadili mtazamo katika zao la korosho kwa kulima mazo mengine mbadala ili kusiwe na utegemezi wa zao hilo la kibiashara badala yake wajikite katika kulima mazao mengine kama ufuta, karanga na mahindi kama mbadala wa zao la korosho ili kukuza uchumi wa mtu moja mmoja.