Radio Fadhila

Matendo mema yawe endelevu na si wakati wa Kwaresma, mwezi Ramadhan tu

30 March 2024, 11:14 AM

Waumini wakipokea neno kutoka Kwa Mchungaji Kikoti

Mchungaji wa kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania KKKT Dayosisi ya kusini mashariki Mch Joseph Kikoti ametoa rai kwa waumini kuendelea kutenda matendo mema hata inapokwisha kipindi Cha kwaresma na mwenzio mtukufu

hayo ameyasema wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na Mkuu wa wilaya ya Mtwara Bi Mwanahamisi Munkunda

Mch Kikoti amesema kuwa matendo mema yanayofanyika katika kipindi hiki yanatakiwa kuwa endelevu Kwa jamii ili kuishi maisha ya kumpendeza Mungu