Radio Fadhila

Mkuu wa wilaya Masasi, viongozi wa dini wakutana apokea maoni

8 June 2023, 9:49 AM

Mkuu wa wilaya ya Masasi Lauter Kanona amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali wa kimila na kidini ndani ya wilaya hiyo, mazungumzo yaliyolenga  kujitambulisha  mbele ya jamii hiyo na kupokea maoni mbalimbali kutoka kwao.

Miongoni mwa mambo ambayo yamejadiliwa katika mkutano huo, ni pamoja na suala la elimu na unyago.

Katika suala la elimu, jamii imetakiwa kutopuuza suala la kuchangia chakula shuleni ili kuwafanya watoto waweze kusoma vizuri na kupelekea kuongeza ufaulu. Aidha Kanoni akizungumza katika mkutano huo pamoja na mambo mengine ametumia nafasi hiyo kutoa kauli ya kuruhusu unyago kufanyika wilayani humo huku akitoa tahadhari ya umri wa watoto kupelekwa katika shughuli hizo za unyago walau kuanzia miaka 8  na kuendelea kwa kusema: