Radio Fadhila

Jela miaka 30 Kwa kosa la kumbaka mwanafunzi wake

4 April 2024, 11:56 AM

mwalimu mbaroni Kwa kumpaka mwanafunzi

Mahakama ya Wilaya ya Masasi mkoa wa mtwara amehukumu kifungo Cha miaka 30 jela Nestory Michael (23) mkazi wa wilaya ya Masasi ambaye ni mwalimu wa shule ya msingi mkalapa Kwa kosa la kumpaka mwanafunzi wake mwenye umri wa miaka 13 ambaye ni mwanafunzi wa darasan la saba katika shule ya msingi mkalapa.

akisoma hukumu hiyo hakimu mkazi Mfawaidhi wa mahakama hiyo Bwn Batista Kashusha ameeleza kuwa mahakama imeridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa jumuhuri ambao umethibitisha mashitaka dhidi ya mshtakiwa pasipo shaka lolote

Hakimu Kashusha amedai kuwa wakati wa usikikizwaji wa shauri hilo ambalo ni kesi namba 16/89 ya mwaka 2023,upande wa jamuhuri ulikuwa na mashahidi saba na vielelezo

na kutokana na ushahidi huo Kwa upande wa jamuhuri na mahakama kujiridhisha na ushahidi huo mahakama imemtia hatiani mshtakiwa Kwa kosa la ubakaji Kwa kifungo Cha miaka 30 jela.

Mbaroni Kwa kumbaka mwanafunzi wake