Radio Fadhila

Nanyumbu imezindua rasmi mpango wa utekelezaji wa kunusuru kaya masikini

21 Aprili 2021, 11:57 mu

HALMASHAURI ya wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara imezindua rasmi mpango wa utekelezaji wa kunusuru kaya masikini kupitia mfuko wa maendeleoya jamii (TASAF III) kipindi cha pili, awamu ya tatu.Mpango huo ulizinduliwa jana wilayani Nanyumbu katika kikao kazi cha kujenga uwelewa wa wadau kuhusu sehemu ya pili ya awamu ya tatu ya TASAF.

taarifa ya utekelezaji huo wa kunusuru ya kaya masikini imesema kuwa serikali baada ya kukamilika kipindi cha kwanza.serikali ya Jamuuri ya muungano wa Tanzania iliendelea na kipindi cha pili katika awamu ya tatu TASAF III ili kaya zote zinazoishi katika mazingira duni zipate usaidizi wa serikali.

Imeeleza kuwa kipindi cha pili cha awamu ya tatu mfuko huo wa maendeleo ya jamii TASAF itafikia zaidi ya kaya 1.4 milioni zenye takribani watu zaidi ya milioni saba kote nchini ikiwa ni nyongeza ya kaya zaidi ya laki tatu na nusu.

chanzo Hamisi Abdelehemani Nasiri